Uingereza yasema Urusi inahaha kuendelea vita nchini UkraineUingereza yasema Urusi inahaha kuendelea vita nchini Ukraine




Ripoti ya jeshi la Uingereza imesema ukosefu wa wanajeshi wa kutosha unaweza kukwamisha maendeleo ya Urusi katika operesheni zake kwenye ukanda wa Donbas mashariki mwa Ukraine, wakati huo huo jeshi la Ukraine likijibu mashambulizi ya Urusi. 

Wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema tangu mwanzoni mwa uvamizi wake, Urusi imehangaika kuendesha mapigano na yumkini tatizo hilo likakithiri. Imesema hivi sasa Urusi inatumia vikosi vya matawi sita ya kijeshi ambayo kwa kawaida kila moja linajitegemea. 

Hata hivyo, vyanzo nchini Ukraine vinaeleza kuwa Urusi imesonga mbele na kukamata maeneo mapya katika mkoa wa Donetsk, ukiwemo mji wa Pokrovske uliopo umbali wa kilomita 10 kituo muhimu cha usafiri cha Bakhmut. Msitari unaounganisha Bakhmut na miji mingine ya Siversk na Soledar ndio ngome ya sasa ya jeshi la Ukraine kuilinda miji mikubwa ya Slovyansk na Kramatorsk.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad