Ukiacha Ustaa Alionao ila Lulu Diva ni Binadamu, UTU na Uaminifu ni Nadra sana Siku Hizi



Siwezi sema ni kosa ama si kosa moja kwa moja, maana huyu pia ni binadamu mwenye faragha zake, ustaa ni vazi tu ambalo limevaliwa na wachache kwenye jamii yetu kutokana na kazi zao zinazo wapa umashuhuri, ila mbali na vazi hilo, hawa pia ni binadamu wenye mioyo na hisia kama binadamu wengine, wanaumia na kufurahi kama wengine. Uwenda likawa kosa sababu Video ipo mtaani, lakini si kosa kama dhamira haikuwa hiyo. (Sina maana video ninayo😁)


Huwezi mlaumu yeyote kwenye hili, aliye jirekodi alitaka amfurahishe mpenzi wake kwa nia njema tu, aliyetuma kwa Mange naye aligeuza ni fursa yake ya kupata pesa, na aliyeiweka hadharani (Mange) naye alitaka apate pesa pia, na wanao isambaza, ndio furaha yao kwenye mambo kama haya, hivi ndivyo tunavyo ishi kwenye ulimwengu wa sasa, kikubwa ni kuwa tahadhari kubwa anza nayo mwenyewe.


NB: UTU na Uaminifu ni nadra sana siku hizi, na unapatikana kwa wachache wasio na alama pia, ikiwa hakuna ulazima wa kufanya hivyo, ACHA!

By Sajo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad