Utata Kifo cha Rais Dos Santos Maiti Yake Kuchunguzwa, Mawakili Watoa Tamko Zito



Rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo dos Santos

MAHAKAMA mjini Barcelona imeidhinisha uchunguzi wa mwili wa aliyekuwa Rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos ufanyike.

Alifariki katika jiji la Barcelona, Hispania siku ya Ijumaa, alikokuwa ameenda kwa matibabu. Uchunguzi wa maiti uliombwa na binti yake na marehemu dos Santos, aitwaye Tchize dos Santos.

Amezungumzia njama ya kumuua babake ili kumzuia kuunga mkono upinzani katika uchaguzi ujao wa Angola.

Rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo dos Santos ameongoza Taifa hilo kwa Takribani miaka 40

Mawakili wa familia ya Dos Santos wameshutumu hatua za serikali ya Angola kurudisha mwili wa marehemu Angola kwa mazishi ya kitaifa, dhidi ya matakwa ya Rais huyo wa zamani kuzikwa kwa faragha nchini Uhispania.


 


Dos Santos alikuwa Rais wa Angola kwa karibu miaka 40, hadi mwaka 2017, alifariki dunia Ijumaa, Julai 8, 2022 nchini Hispania

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad