Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema kwamba nyongeza ya mshahara ya kima cha chini cha asilimia 23 ya mshahara wa watumishi wa umma, iliwahusu zaidi wafanyakazi wenye kipato cha chini na kwamba wapo ambao hawajapata asilimia hizo.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Julai 29, 2022, jijini Dodoma, na kusema kwamba licha ya kwamba licha ya nyongeza ya mishahara iliyotolewa haikidhi lakini bado serikali inayo dhamira ya dhati ya kuendelea kuongeza mishahara ya watumishi wake.
"Ukiangalia mshahara kama wa Mawaziri wamepata 0.7%, sasa nani amepata hiyo ni yule mwenye kipato kikubwa, ujumbe wa msingi ni kwamba asilimia 23 iliyotamkwa haijalipa watu wote," amesema waziri Mkuu.