Wanafunzi Waomba Kuishi Shuleni na Watoto wao



Kutokana na kukosa umakini darasani, baadhi ya wanafunzi waliorejea shuleni baada ya kukatisha masomo kutokana na ujauzito, wameomba kujengewa hosteli zitakazowasaidia kuwa karibu na watoto wao.


Ombi hilo limetolewa kwa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia (WB), Dkt. Victoria Kwakwa katika ziara yake aliyoifanya Shule ya Msingi Turiani kufuatilia utekelezaji wa mradi wa kuwarejesha masomoni wanafunzi waliokatisha masomo kutokana na matatizo mbalimbali, ikiwamo ujauzito.


Mbali na ombi hilo, pia wameomba kuboreshewa miundombinu ya kujifunzia ili waondokane na mfumo wa kusoma kwa nadharia hali itakayowasaidia kumudu ushindani wa kusoma na kuelewa.


“Kwa sababu tunatoka mbali, tunafika nyumbani tumechoka na tunakosa muda wa kusoma tunaomab kujengewa hostel hii itatusaidia kuwa karibu na watoto wetu kwa sababu wakati mwingine tunakosa umakini darasani kutokana na mazingira tuliyowaacha watoto wetu,” alisema mmoja wa Wanafunzi hao.


Hata hivyo, Dkt. Victoria amesema wataendelea kushirikiana na Wizara ya Elimu ili kufanya maboresho yatakayowezesha wanafunzi wengi kurudi darasani na kuendelea na masomo yao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad