Wanaume kushuhudia wenza wao wakijifungua CCBRT




Dar es Salaam. Wakati hospitali ya CCBRT ikizundua rasmi jengo lake la huduma ya afya ya mama na mtoto, imetenga vyumba ambayo wenza wa wajawazito wataweza kuwashuhudia wakiwa wanajifungua.

Hayo yamesemwa leo Jumanne Juni 5, 2022, na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Brenda Msangi kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo hilo.

Akielezea kuhusu mradi huo ambao umegharimu zaidi ya Sh101.2 bilioni, Brenda amesemna vyumba hivyo nane vya kujifungulia ambavyo wenza wanaweza kushuhudia wake zao wakiwa wanajifungua.

“Ndani ya jengo hili pia kuna vyumba nane, ambavyo mama anayejifungua anaruhusiwa kuingia na msaidizi mmoja atakayemchagua yeye wakati wa kujifungua.


 
“Iwe mume wake, iwe dada, mama na hii Mheshimiwa Rais ile sababu ambayo kina baba walikuwa wanajificha sasa tunaenda kuifanyia kazi,”amesema Brenda.

Mkurugenzi huyo amesema jengo hilo lina vitanda 140 vya kulaza kina mama na kati ya hivyo vitanda 50 vimeunganishwa na mfumo tiba hewa ’Oxgen’.

“Pia vipo vitanda 46 kwa ajili ya watoto wachanga na tunacho kitengo maalumu cha watoto wa wagonjwa maalumu, kitengo cha usafi wa vyombo vya matibabu na upasuaji.

“Kitengo maalumu cha upasuaji na maabara zenye vifaa vya kisasa, na vyumba 15 vya wagonjwa wa nje ambavyo vitawezesha kuhudumia wagongwa wa nje 300 kwa siku,”ameeleza Brenda.

Hata hivyo amebainisha kuwa lengo kubwa la kuanzishwa kwa jengo hilo ni kutaka kuwahakikishia wazazi wote uzazi salama.

“Huu ni uwekezaji mkubwa na dhamira ya dhati ya CCBRT, Serikali yetu na wafadhili katika kuhakikisha tunanusuru maisha ya mama zetu na watoto wachanga, hivyo sisi kama ccbrt tunawahakikishia kutoa huduma bora kwa watanzania wenzetu wenyewe mahitaji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad