Watu 20 Wakutwa Wamefariki Jangwani Nchini Libya, Chanzo Chabainika




WATU 20 wamekutwa wakiwa wamefariki katika jangwa nchini Libya sababu kuu ikiwa ni kutokana na kiu baada kukosa maji kwa muda mrefu huku kukiwa na wasiwasi kuwa watu hao yawezekana walikuwa wamepotea.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Libya ni kwamba miili hiyo iligunduliwa na Dereva wa magari ya masafa marefu na inadaiwa kuwa miili hiyo imegunduliwa baada ya watu hao kupotea kwa muda wa zaidi ya wikli mbili


Waokoaji wakiendelea kuokoa miili ya watu walifariki Jangwani nchini Libya
Dereva huyo anadaiwa kuigundua miili hiyo wakati anasafiri kukatiza Jangwa hilo umbali wa kilomita 320 Kusini Magharibi mwa Kufra na Kilomita 120 kutoka mpaka wa Chad.

“Dereva alipotea na tunaamini kundi lilipotea na kufia jangwani siku 14 zilizopita tangu mara ya mwisho yafanyike mawasiliano ya simu ni Juni 13.” Alisema Afisa wa Ambulance wa Kufra, Ibrahim Belhasan kupitia njia ya simu.


 

Chanzo cha kifo chao kinaaminika kuwa ni kiu kutokana na kukosa maji Jangwani
Miili miwili ilikuwa ni ya raia wa Libya na iliyobaki inaaminika kuwa ni ya raia wa Chad ambao walikuwa wanavuka Jangwa kuingia nchini Libya

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad