Watu 30 wateketea kwa moto Nigeria

 


Mamlaka nchini Nigeria zinasema kwamba takribani watu 30 wameteketea kwa moto na kupoteza maisha huku makumi wengine wakijeruhiwa vibaya katika ajali mbaya ya barabarani iliyotokea Kaskazini kwa mji wa  Kaduna.

Ajali hiyo imehusisha mabasi matatu ya abiria ambayo yalishika moto baada ya kugogana saa za  jioni ya jana kwenye barabara kuu inayounganisha majiji ya Zaria na Kano.


Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani katika jimbo la Kaduna Bw. Hafiz Muhammad amesema kua walioathiriwa na ajali hiyo ni wamama na watoto.


Majeruhi walikimbizwa kwenye hosptali mbili zilizo karibu huku majeruhi wengine wakionekana kuvunjika mifupa.  


Ajali hiyo imetokea  katika eneo ambalo mabasi hutakiwa kupishana ili kupisha ujenzi unaoendelea wa barabara.


Inasemekana madereva hao walikua wanagombania nani awe wa kwanza kupita , ndipo walipogongana na kusababisha mlipuko wa moto.


Ajali za barabarani zimekua kawaida nchini humo sababu zikitajwa kuwa ni miundombinu mibovu ya barabara , mwendo kasi, magari mabovu na kutotii sheria za usalama barabarani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad