Waziri Mkuu Sri Lanka Akaimu Nafasi ya Rais, Wananchi Wamkataa



Spika wa Bunge nchini Sri Lanka ametangaza kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ranil Wickremesinghe ameteuliwa kuwa Rais wa muda wa taifa hilo lililoingia katika mzozo wa kiuchumi



Spika wa Bunge nchini Sri Lanka ametangaza kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ranil Wickremesinghe ameteuliwa kuwa Rais wa muda wa taifa hilo lililoingia katika mzozo wa kiuchumi


Spika huyo amesema Rais Gotabaya Rajapaksa alimfahamisha kuhusu uteuzi huo chini ya Kifungu cha 37.1 cha katiba ya Sri Lanka lakini bado hakuna neno la moja kwa moja kutoka kwa Rajapaksa mwenyewe.


Kwa mujibu wa Katiba ya Sri Lanka, nafasi ya rais ikiwa wazi, waziri mkuu ataapishwa na kukaimu kwa muda mpaka atakapochaguliwa rais kutoka miongoni mwa wabunge ambapo Spika huyo amesema uchaguzi unaweza kufanyika Julai 20, 2022.


Hayo yanajiri wakati ambapo tayari Rais Gotabaya Rajapaksa ameikimbia nchi hiyo kwa ndege ya kijeshi huku maandamano yakiendelea kila kona ya nchi


Serikali imetangaza hali ya hatari nchini humo na kuweka amri ya kutotoka nje kwenye baadhi ya maeneo ya nchi hiyo


Maelfu ya waandamanaji wamepambana na polisi, wakiandamana kwenye ofisi ya waziri mkuu wakimtaka naye aondoke.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad