Waziri Ndumbaro: Katiba iliyopo ina mapungufu



 

WAZIRI wa Sheria na Katiba, Dk. Damas Ndumbaro amesema  licha ya kuwa Katiba iliyopo inafaa lakini ina mapungufu yake ndio maana Serikali imetoa muelekeo wa namna ya kufanya mabadiliko ya Katiba baada ya kupokea mapendekezo ya wananchi. Anaripoti Faki Sosi Ubwa… (endelea).

Dk. Ndumbaro ametoa kauli hiyo leo tarehe 20 Julai, 2022  jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu vipaumbele vya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Waamesema Katiba iliyopo inafaa ijapokuwa ina mapungufu ambayo yatafanyiwa marekebisho.

“Katiba iliyopo inafaa lakini ina mapungufu mimi mwenyewe kama binadamu nina mapungufu kwa hiyo ninaweza nisifae kuwa waziri labda mlete wasiri malaika.


 
“Katiba ya Marekani yenyewe ina mapungufu Supreme Court (Mahakama ya Juu) juzi imetoboa matundu kwenye suala la posho, umesikia Wamarekani wanasema Katiba haifai … Tuyaangalie yale mapungufu tuyajadili ili wenye mamlaka ambao ni wananchi tuyaondoe tunayondoe mapungufu hayo” amesema Dk. Ndumbaro.

Waziri Ndumbaro amesema Serikali imefungua mjadala wa kujadili katiba.

“Tuelimishane, tujue hicho tunachosema hakifai ni nini kifungu kipi na mbadala wake nini kwenye hili serikali imefungua mjadala.


“Hili si suala la wanasiasa mimi kama mwanasiasa ukiniruhusu nitasema kwanini tunafanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano, tufanye miaka kumi kwa kuwa uchaguzi ni gharama hiyo itakuwa hoja yangu lakini je, mwananchi atataka mrejesho wa huo mkataba kwa miaka kumi?  si ataona ni parefu.

“Sasa hivi hatumzuii mtu yoyote kusema Katiba hii inamapungufu tunachotaka na ndio wizara tunafungua mjadala tuambie kifungu, tueleze mapungufu, pia tueleze mapendekezo yako… utakuwa unasaidia mchakato wa kupata katiba mzuri” amesema Waziri Ndumbaro.

Waziri Ndumbaro amesema kuwa mkakati wa Serikali ni kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu Katiba na sheria.

Amesema kuwa ni muhimu wananchi waijue Katiba iliyopo, ajue upungufu na ubora wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad