WCB Wamkaushia Rayvanny...Nguvu Aliyotumia Rayvanny Kuwaanga WCB ni Kubwa Mno Kuliko Ambayo WCB imetumika Kumuaga


Nguvu aliyotumia Rayvanny kuwaanga WCB ni kubwa mno kuliko nguvu ambayo WCB imetumika Kumuaga. Tujikumbushe, wakati Country Boy anaondoka Konde Gang alifanyiwa Party kwaajili wa Kuagwa kwake, huu ndio utaratibu ambao hata kwenye Timu za Mpira mtu akiondoka lazima Timu ioneshwe kuguswa.

Kwa Rayvanny imekuwa tofauti, kijana wa watu ameandaa mpaka Documentary Fupi ili kuwaaga WCB lakini wao wamecomment Kirahisi sana, inaonesha hakuna hata aliyeguswa. Tunaona Babalevo alivyoandika ujumbe mzuri wa kumuaga Rayvanny lakini mpaka sasa Zuchu, Diamond, LavaLava na Mbosso hawajapost lolote kuhusu Rayvanny, Imagine Zuchu amepost Video ya Mbosso "Moyo" ila ameshindwa kupost kuhusu Rayvanny.

Hii inaleta picha mbaya sana, huenda mambo hayapo sawa kama ambayo Rayvanny anajitahidi kutuaminisha, inawezekana kuna ugomvi mzito sana pale, sio bure. Tusubiri tu ipo siku Rayvanny atafongoka ukweli

@hopetygatz 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad