Yanga Yampa Mkono wa Kwaheri Kaseke, Awashukuru Mashabiki kwa Sapoti Waliompa




Kiungo mshambuliaji Deus Kaseke ambaye amepewa mkono wa Kwaheri na klabu ya Yanga
KLABU ya Yanga SC, leo Alhamisi, Julai 14, 2022 imetangaza kuachana na mchezaji wake mwandamizi, Deus Kaseke ‘Mwaisa’ na kumtakia kila kheri aendako.

Katika taarifa fupi ya Yanga isiyozidi maneno 20 imesema; “Umekuwa sehemu kubwa ya mchango wa mafanikio kwenye Klabu yetu, tunakutakia kila la kheri na mafanikio uendako.”

Kwa upande wake, Kaseke kupitia ukurasa wake wa Instagram ameishukuru Yanga kwa kipindi chote ambacho ameitumikia.
“Asante sana Yanga mmekuwa sehemu kubwa saana ya maisha yangu ya mpira, nashukuru kwa sapoti kubwa mlionipa kipindi chote nilichotumikia Timu ya Wananchi, asanteni sana Wananchi.

Kaseke ameitumikia klabu hiyo kwa muda wa zaidi ya miaka mitano akishinda mataji mawili ya Ligi Kuu Tanzania Bara, tetesi zinasema Mnyakyusa huyo anawindwa na walima alizeti Singida Big Stars.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad