Young Africans kuweka kambi Dar es salaam



Wachezaji wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans wanatarajia kurejea Kambini Kesho Jumatano (Julai 20) na Keshokutwa Alhamis (Julai 21), tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2022/23.

Wachezaji wa Young Africans walipewa mapumziko, baada ya kumaliza msimu wa 2021/22 Jumamosi (Julai 02), kwa kucheza mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ dhidi ya Coastal Union, uliopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Msemaji wa Young Africans Haji Sunday Manara amezungumza na Waandishi wa Habari leo Jumanne (Julai 19) jijini Dar es salaam na kuanika mipango na mikakati ya kuanza kwa kambi ya kikosi chao.


Manara amesema Kambi ya Kikosi chao itakua Kigamboni jijini Dar es salaam {AVIC Town}, baada ya kufutwa kwa Kambi ya nchini Uturuki, ambayo ilitarajiwa kuanza mwishoni mwa juma lililopita.


Amesema maamuzi ya kufutwa kwa Kambi ya Uturuki, yamekuja baada ya Uongozi kupokea ushauri kutoka Benchi la Ufundi la klabu hiyo, ambalo lilihitaji wachezaji kuwa na muda mrefu wa mapumziko baada ya kuwa na msimu mrefu wa mafanikio.

“Tulipanga likizo yetu kumalizika tarehe 15/07/22 Makocha wakashauri tuwaongezee Wachezaji wetu muda wa mapumziko kwasababu walikuwa na msimu mrefu na hawakupata nafasi ya kupumzika kutokana na majukumu ya Klabu na timu za Taifa”

“Tumekubaliana Camp yetu ya Pre season iwe Dar es Salaam, tutakwenda Avic Town, tuna facilities za kutosha, tumeongeza vifaa vingine maalum kabisa kwa ajili ya Pre Season Camp na tumewapa wachezaji wetu muda mrefu kidogo wa mapumziko, wachezaji wataanza kuingia kambini Julai 21,” amesema Haji Manara

Young Africans inatarajia kucheza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC Agosti 13, ambao utaashiria kufunguliwa rasmi kwa msimu mpya wa 2022/23.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad