Mkoa wa Njombe umepokea wawekezaji kutoka Falme za Kiarabu, wenye lengo la kuwekeza kwenye uzalishaji wa Parachichi, Macademia nuts pamoja na uwekezaji katika sekta ya utalii, yakiwa ni matunda ya filamu ya The Royal Tour iliyofanywa na Rais Samia.
Kulia ni Rais Samia Suluhu Hassan, na kushoto ni wawekezaji kutoka nchi za Falme za Kiarabu
Katibu Tawala wa mkoa wa njombe Judica Omary, amesema kufika kwa wawekezaji hao mkoani Njombe, kunaenda kufungua uwanja mpana wa masoko wa zao la Parachichi.
Kwa upande wake Mbunge wa Afrika Mashariki Fensi Haji Mkuhi, amesema kuwa licha ya wao kuwa na wajibu wa kutunga sheria pia wanalo jukumu la kushawishi wawekezaji kuja kuwekeza nchini hususani mkoani Njombe ambako ndio wazalishaji wakubwa wa zao la Parachichi.
Kwa upande wao wamiliki wa makampuni Bakoin wamesema kutokana na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na filamu ya Royal Tour, kumewapa hamasa ya kuunga juhudi za Rais katika kuvutia wawekezaji