Zoran asuka benchi kibabe, kuleta mtaalam wa USM Alger




Kocha Mkuu, Zoran Maki ameanza kusuka benchi la Simba kibabe kwa ajili ya kufanya navyo kazi ndani ya Msimbazi.

Mwanaspoti lilikuwa la kwanza kukujuza mashine mpya saba ambazo Simba imesajili, Moses Phiri aliyetambulishwa tayari, Cecar Lobi Manzoki, Victor Akpan, Nassoro Kapama, Nelson Okwa, Augustine Okra na Habib Kyombo

Ukiachana na hilo mabosi wa Simba walimpa kazi nzito kocha mpya, Zoran kutafuta wasaidizi wawili atakaokuja nao kwenye kambi ya timu hiyo itakayokuwa Misri kuanzia Julai 15 kwa maandalizi ya msimu mpya (pre-season).

Katika kuhakikisha Simba inakuwa na benchi la ufundi imara, Zoran anatakiwa kutua Misri akiwa na wasaidizi wake wawili ambao ni kocha wa makipa pamoja na wa viungo.


 
Simba kwa sasa haina kocha wa makipa baada ya kuachana na Tyron Damons aliyepata kibarua kingine Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, huku pia ikiachana na kocha wa viungo, Mhispania Daniel De Castro.

Mwanaspoti limepenyezewa kuwa tayari ana majina mawili ya makocha atakaoenda nao kambini  mmoja akiwa ni kocha wa makipa Mohamed Haniched aliyewahi kufundisha USM Blida, USM EL Harrach na USM Alger ambazo zote zinatoka nchini kwao Algeria.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza Zoran atakuja na kocha wa viungo anayetambulika kwa jina la Kareem Bayey ambaye anaelezwa amekuwa naye kwenye timu nyingi alizofundisha huko nyuma.

Zoran inaelezwa anavutiwa zaidi na kocha huyo wa viungo kwani mbali ya uwezo wake huo amekuwa pia akimsaidia kama kocha msaidizi ndio maana kila anapokwenda kufundisha anakuwa pamoja naye.

Mabosi wa Simba wamekubaliana na mapendekezo ya wasaidizi hao wa Zoran atakaokuwa nao kwenye kambi ya timu hiyo Misri.

Simba inaendelea kusuka kikosi matata kabisa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad