16 waliofariki ajali ya Kahama watambuliwa



Shinyanga. Miili ya watu 16 kati ya 20 waliofariki kwenye ajali iliyotokea eneo la Mwakata Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga imetambuliwa na kuchukuliwa na ndugu tayari kwa mazishi.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Leonard Nyandahu, miili ya watu wanne waliofariki kwenye ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia Agosti 9, haijatambuliwa na inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Wilaya ya Kahama.

Amewataja waliotambuliwa kuwa ni Kano Lutema (48), Jonas Kija (49), Paul Choyo (23), Tungu Magega (65), Salinja Bukelebe (28), Sarah Siti (46),  Nuhu Mpinga (28), Augustino Mnyamba (28) na Musa Ally (25), wote wakazi wa Manispaa ya Kahama.

Wengine ni Leonard Mbasu (52), mkazi wa Manispaa ya Shinyanga, Sebastian Kimaro (28), na Julius Jeremia (28), wote wakazi wa jiji la Mwanza.


Kaimu Kamanda Nyandahu amewataja marehemu wengine waliotambuliwa kuwa ni Erick Peter (31), mkazi wa Masumbwe Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, Flora Wilson (28), Aman Silus (35), mkazi wa Kahama na Nicolous Budole (34), mkazi wa Didia Wilaya ya Shinyanga.

Akizungumzia hali ya majeruhi 15 wa ajali hiyo iliyohusisha magari matatu na trekta, Mganga Mfawidhi Hospitali ya Manispaa ya Kahama, Dk Deogratias Nyanga amesema wagonjwa watano wamepewa rufaa kwenda hospitali mbalimbali kwa ajili ya matibabu zaidi.

“Wagonjwa watatyu wamepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, mmoja amepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga huku mgonjwa mmoja amehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete kwa ombi na ushauri wa ndugu zake,” amesema Dk Nyanga


Amesema wagonjwa 10 waliosalia hospitalini hapo wanaendelea vema nab ado wako chini ya uangzalizi wa karibu wa wataalama wa afya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad