Wakili Ahmednasir Abdullahi amemwonya Rais mteule William Ruto kujihadhari na Rais Uhuru Kenyatta kesi ya uchaguzi ikielekea mahakamani
Kwa mujibu wa Ahmednasir, Rais Kenyatta ndiye adui wa Ruto na wala sio kiongozi wa ODM Raila Odinga
Ahmednassir anadai kuwa Uhuru amekuwa akijiandaa kwa vita katika Mahakama ya Upeo kwa miaka mitatu sasa
Wakili matata Ahmednasir Abdullahi sasa anadai kuwa adui wa Rais mteule William Ruto ni Rais Uhuru Kenyatta na wala sio kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga.
Ahmednassir Aonya Ruto Vita vya Uchaguzi Vikielekea Mahakamani: "Adui Yako ni Uhuru si Raila"
Wakili Ahmednasir Abdullahi amedai kuwa Rais Uhuru Kenyatta ndiye adui wa William Ruto na wala sio Raila Odinga.
Kupitia kwa ujumbe kwenye mtandao wa Twitter, Ahmednasir alimtaka Ruto kutojilegeza na kuwa makini kuhusu Mahakama ya Upeo itakavyoshughulia kesi ya kupinga ushindi wake wa uchaguzi wa urais.
Kwa mujibu wa wakili huyo, vita vya Ruto ni dhidi ya Uhuru ambaye amekuwa na tofauti naye kwa muda mrefu, Ahmednassir akidai kuwa Uhuru amekuwa akijiandaa kwa vita katika Mahakama ya Upeo kwa miaka mitatu sasa.
"Nitamheshimu Rais Akistaafu": William Ruto Aahidi Kumchunga Uhuru
“Rais mteule William Ruto anapaswa kujua kuwa katika Mahakama ya Upeo kama tu uchaguzi wa Agosti 9, Rais anayeondoka Uhuru Kenyatta ndiye adui wake wala sio Raila. Baada ya kushindwa mara moja, Uhuru sasa anataka kubadili mkondo katika Mahakama ya Upeo. Kumbuka Uhuru alijiandaa kwa vita hivi miaka mitatu iliyopita,” Ahmednassir alisema kupitia kwa ujumbe kwenye mtandao wa Twitter.
Mgombea wa urais wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga ambaye aliungwa mkono na Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuwasilisha kesi katika Mahakama ya Upeo kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais ambapo Ruto alitangazwa mshindi.
Raila alisema hatambui hatua ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kumtangaza Ruto kuwa Rais mteule.
“Mtu yeyote asichukue sheria mikononi. Tunatumia mbinu zote za kikatiba kubatili tangazo haramu la Chebukati. Tuna uhakika kuwa haki itatendeka,” Raila alisema.