RAIS wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud Jumanne ameahidi kulitokomeza kabisa kundi la Al Shabab katika taarifa aliyoitoa kwa taifa tangu wanamgambo hao wa Kiislamu kufanya shambulio baya kwa uvamizi uliodumu kwa saa 30 kwenye hotel ya Hayat mjini Mogadishu.
Shambulio hilo limekua kubwa zaidi katika mji mkuu wa Somalia tangu Rais huyo aingie madarakani. Kundi hilo ambalo lina uhusiano na kundi lingine la kigaidi la Al Quaida limekua likisababisha maafa mengi katika nchi ya Somalia, Kundi hilo limekua likifanya mashambulio ya kujitoa muhanga katika sehemu za kijamii.
Hotel iliyoshambuliwa na kundi la Al Shabaab
Katika uvamizi wa kundi hilo ulioanza ijumaa umesababisha vifo vya watu 27 na watu zaidi ya 117 wakiwa majeruhi. Katika waliokufa kuna raia wa Norway pia ambao walikuwepo katika hoteli hiyo ya Hayat kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na serikali ya Norway.
“Ninajua kwamba wananchi wa Somalia wamechoshwa na rambirambi na maombolezo yasiyoisha, najua kwamba mnawapoteza watu wenye thamani katika kila shambulio linolafanywa na magaidi,” Mohamud amesema.
“Tuna dhamira ya kuwadhoofisha magaidi wanaoteketeza wanainchi wetu hadi maeneo yote wanayoyadhibiti yamekombolewa, hili ni jambo la kipaumbele kwa serikali yetu na maandalizi na utelekelezaji wa mpango huo unaendelea,” amesema bila kufafanua zaidi.
Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao