Album ya ‘Made In Lagos’ ya Wizkid inazidi Kuchanja Mbuga Sokoni...Yagonga Gold


Album ya ‘Made In Lagos’ ya Wizkid inazidi kuchanja mbuga sokoni. Album hiyo imefikisha mauzo ya Gold sokoni, ikiwa na maana tayari imeshauza kopi laki tano nchini Marekani tangu ilipotoka Oktoba 30, mwaka 2020.


Kutokana na hatua hiyo chama cha Recording Industry Association of America (RIAA) kimemkabidhi cheti maalum Wizkid kufikia mafanikio hayo. Hivyo Wizkid anakuwa mwanamuziki wa kwanza mwenye ya asili ya Nigeria kuwahi kufikisha idadi hiyo ya mauzo katika soko la muziki la Marekani.


Ikumbukwe, "Made In Lagos" ni album ya nne ya Wizkid na ilitoka chini ya usimamizi wa kampuni za Starboy Entertainment na RCA Records.


Aidha, kwa sasa Wizkid anajiandaa kutoa album yake ya tano aliyoipa jina "More Love Less Ego – MLLE" ambayo aliahidi mashabiki zake kwamba itatoka tarehe ya mwisho ya ziara yake inayoendelea hivi sasa ambapo itakuwa ni Disemba mwaka huu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad