Aliyeambukizwa Ukimwi Kulipwa Shilingi Milioni 300


Mwigizaji maarufu duniani Charlie Sheen amekubali kumaliza kesi ya madai iliyomkabili kwa muda mrefu kwa kulipa USD Dola laki mmoja na elfu ishirini [Tsh Milioni 300]. Mlalamikaji atapewa pesa hizo ndani ya miezi 12, ikiwa ni dola elfu 10 kila mwezi.

Mlalamikaji kwenye kesi hii alidai kuwa aliambukizwa UKIMWI Na Charlie Sheen baada ya kufanya nae ngono bila kinga. Kesi hii imemalizwa nje ya mahakama sababu hapakuwa na ushahidi kuwa Charlie alijua hali yake muda huo.

Tambua Nov 17,2015 Charlie Sheen alitangaza rasmi kuwa ana UKIMWI baada ya kuficha hali yake kwa muda mrefu na hata kulipa watu pesa ili wasivujishe taarifa hizo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad