Aliyeporwa Ranger Rover na Makonda Alipuka, Amuangukia Rais


MFANYABIASHARA Patrick Christopher Kamwelwe mkazi wa New York nchini Marekani ameshusha tuhuma nzito dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Tuhuma hizo zinahusu madai ya kumpora gari lake aina ya Ranger Rover na kuibandika namba za RC DSM (Mkuu wa mkoa Dar es Salaam) kipindi akiwa kwenye wadhifa huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kamwelwe ambaye pia anajulikana kwa jina maarufu kama PCK amedai Makonda anaendelea kuitumia gari hiyo hata baada ya kuondolewa madarakani licha ya kwamba si mali yake halali.

Akizungumza na Raia Mwema katika mahojiano maalum Kamwelwe ambaye ni mzaliwa wa Mpanda mkoani Katavi aliyekuwa akiishia jijini Dar es Salaam kabla ya kukimbilia Marekani kutokana na vitisho, amedai kwamba baada ya kufuatilia ili arejeshwe gari hiyo nyeusi yenye thamani ya Sh milioni 220, ndipo vitimbi na vitisho vilipoanza na kubambikiwa kesi ya jinai kwa kumiliki mali haramu.

Alidai kutokana na tuhuma hizo Juni 2017 alifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku akaunti zake za benki pamoja na mali zake zikishikiliwa hadi sasa.

GARI ILIVYOKWAPULIWA

Kamwelwe ambaye awali alikuwa mfanyabiashara wa magari, msanii wa Bongofleva na promota wa muziki, alisema mwaka 2017 alifuatwa na mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu, Samwel Malecela, William Malecela maarufu kwa jina la Lemutuz na kumueleza kuwa Makonda…. kwa taarifa zaidi soma gazeti la Raia Mwema la leo tarehe 31 Agosti, 2022.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad