1: WOW. JUST WOW .. WHAT A MATCH🙌 TUMEENJOY SOKA. Siku zote, Mechi ya wazi, Mechi isiyokuwa na mitego, Mechi isiyokuwa na mipango mingi ya kukaba.. Ni Burudani kwa watazamaji wa Soka
2: POINTI 6. Mabao 5. CLEAN SHEET 2 Mfululizo.. Kubwa zaidi ‘Lete Mzungu’, Dejan Georgijević Ameleta Burudani.. What A Moment.. Mashabiki wa Simba wapewe Ulinzi😀
3: Tactically, Kocha wa Simba, Zoran Maki ni sawa Kilema aliyejua mwendo upi sahihi kwake.. Hana kiungo mzuri mkabaji.. Nini unafanya? Wekeza nguvu kwenye kushambulia
4: Simba wana wachezaji wazuri sana kwenye 1v1 .. Babu Zoran amechagua kuanza na Kanoute chini, kisha kuweka watu watano mbele wenye akili ya kushambulia.. Hapa anatega mpinzani kulazimisha kufungua mchezo. Kivipi?
5: Ni rahisi kufika kwenye 18 ya mwisho. Ukienda mara moja, ukirudia mara mbili.. Ujumbe unaokwenda kwa koch wa timu pinzani ni kupunguza tahadhari na kutamani kushambulia zaidi.. Mechi ikiwa hivi, QUALITY HUAMUA✅
6: CHAMA NI SANAA YA SOKA! Anachoweza kufanya Rutto kwenye Jukwaa la Siasa, Chama anaweza kukifanya mara mbili yake uwanjani.. Ni mjuzi. Mtaalam. Anakupa usichokitarajia🤝 ASANTE CHAMA
7: ‘Finishing’ nzuri kwa Dejan.. Mwili wake ulimfanya dhambi ya uongo kwa golikipa. Alidesh kulia akageuka kushoto.. Kamba nzuri na mguu wa kushoto.. Hii itampa kujiamini zaidi
8: Bado Simba inawadai zaidi BANDA na SAKHO.. Wana kasi, skills nzuri za kuvamia eneo la mwisho Lakini Maamuzi yao bado sio sahihi kwenye kuamua mchezo
9: Well Done kipa wa Kagera👏 Licha ya kosa la mawasiliano kati yake na mabeki, alikuwa na mechi bora sana kwenye Saves. Utulivu mkubwa sana kwenye Timing zake kuhesabu hatua za mastraika
10: Asante Outtara! BEKI WA SOKA. Asante Kanoute.. Well Play Makame.. Asante pia Beki Laurent.. Kagera wana Timu nzuri sema wamepata ratiba ngumu mwanzoni
Nb: Mzungu ahesabiwa kwenye SENSA 😀