Amuuwa Baba yake kwa Kuoa Mke wa Pili

 


Polisi nchini Nigeria inamtafuta mtu mmoja wa makamo Kazeem Muhammed, baada ya kumuuwa baba yake na kukimbia kusikojulikana akimtuhumu kuoa mke wa pili.


Kazeem anadaiwa kutenda kosa hilo la mauaji katika eneo la Kwankashe Suleja, Jimbo la Niger baada ya kukasirishwa na baba yake kwa kuoa mke wa pili zaidi ya mwaka mmoja uliopita akimtuhumu kuongeza ugumu wa masha na kukosekana kwa furaha nyumbani.


Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Trust, kaka wa marehemu, Isah amesema mara baada ya kutokea kwa mzozo huo Kazeem alimshambulia baba yake kisha kumuua na alikimbia na kwamba Polisi bado inaendelea na msako ili kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha Mahakamani.


Waombolezaji waliokusanyika katika eneo la tukio la Kwankashe Suleja, Jimbo la Niger. (Picha na Within Nigeria)

Isah mesema, “Mvulana huyo ni mraibu wa dawa za kulevya na huwa anajihusisha na vitendo viovu na walipokuwa wakizozana asubuhi, alibeba ubao na kumpiga babake ambaye alianguka sakafuni na alipogundua haamki alikimbia ndipo tukamuwahisha kaka yangu hospitali, lakini alifariki baadaye.”


Aidha alisema suala hilo limeripotiwa kwa mamlaka husika huku mabaki ya kaka yake yakiwa yamezikwa kwa mujibu wa taratibu za dini ya Kiislamu huku Polisi katika eneo hilo wakikataa kuzungumzia tukio hilo kwa kuwa hawana mamlaka kwa mujibu wa Utaratibu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad