Jiwe lililopatikana kwenye machimbo nchini Angola
WACHIMBAJI wa migodi kaskazini mashariki mwa Angola, wamegundua Almasi kubwa ya aina yake ambayo haijawahi kugunduliwa katika miaka 300.
Operata wa tovuti wa Australia ameliita kuwa ni jiwe la karati 170 The Lulo Rose,imesema Almasi hiyo itauzwa kwa zabuni ya Kimataifa ya Kampuni ya Uuzaji wa Almasi ya Angola .
Machimbo katika Migodi nchini Angola
Upatikanaji wa Almasi katika Mugodi wa Lulo umekaribishwa na Serikali ya Angola.
Waziri wa Rasilimali na Madini wa Nchi ya Angola amenukuliwa akisema:
“Rekodi hii ya Almasi ya kuvutia ya Walidi inayopatikana kutoka Lulo inaendelea kuionyesha Angola kama Mhusika muhimu katika jukwaa la Dunia la Uchimbaji wa Almasi.”
Mawe ya madini nchini Angola yanauzwa kwa bei ghali sana
Aidha Waziri huyoanayefahamika kwa jina la Diamantino Azevedo alisema katika taarifa yake kuwa mawe kama hayo baada ya kukatwa na kung’olewa yameuzwa kwa bei iliyovunja rekodi.
The pink star na Almasi ya Walidi za karati 59, zimeuzwa kwa Dola milioni 71.2 Mnamo Mwaka 2017 ambayo ni ghali zaidi iliyoweka rekodi ambayo haijawahi kutokea Nchini humo.