Askofu Kilaini alaani Klabu ya Simba kutumia msalaba kwa dhihaka




ASKOFU Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Methodius Kilaini amelaani kitendo cha klabu ya Simba kutumia msalaba kufanya dhihaka na kusema ni “dharau na kufuru kubwa kwa waamini wakristu na wote wanaoamini walikombolewa katika msalaba huo.”


Itakumbukwa kuwa katika tamasha la Simba Day lililofanyika jana Jumatatu tarehe 8 Agosti, 2022, msaani Tunda Man aliingia katika uwanja wa Benjamini Mkapa akiwa amebebwa katika jeneza pamoja na msalaba uliokuwa na maneno ya dhihaka kwa watani wao wa jadi Yanga yaliyosomeka “Kifo cha Utopolo.”



Askofu Kilaini amesema katika andiko lake kwenye akaunti yake ya Facebook kuwa “tendo hili ni kufuru kwa ishara zilizotakatifu kwa Imani yaani Msalaba. Kutumia msalaba kudhihaki ni dharau na kufuru kubwa kwa waamini wakristu na wote wanaoamini kwamba walikombolewa katika msalaba huo.

Ameendelea kusema “ni tusi kubwa kwao.”

Mbali na matumizi ya msalaba pia amelaani uvaaji wa mavazi yanayofanana na yale yanayovaliwa katika ibada takatifu na kusema “ni kuzifanya ibada za Kikristo kichekesho. Inasikitisha sana. Sikutegemea tumefikia hatua hiyo.”


Askofu Kilaini amesema ni matumaini yao kuwa uongozi wa Klabu ya Simba utalaani kitendo hico na kuomba msamaha kwa waamini wakristo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad