Kikosi cha wanasheria wa muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya kimewasilisha kesi yao ya kupinga ushindi wa Rais Mteule William Ruto, kwa ufupi
Siku ya Jumatatu, viongozi wa Azimio waliwasili katiak Mahakama ya Upeo wakiwa na rundo la ushahidi lilojaa kwenye lori, ila imewalazimu kupunguza ushahidi huo hadi kurasa 40
Fred Orego ambaye ni mmoja wa wakili katika kesi hiyo alisema kupunguzwa kwa stakabadhi za kesi hiyo hadi kurasa 40, inaendana na sheria za mahamakama hiyo
Kikosi cha wanasheria wa muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya kimewasilisha kesi yao ya kupinga ushindi wa Rais Mteule William Ruto, kwa ufupi.
Azimio Yapunguza Ushahidi Wake Hadi Kurasa 40 Baada ya Kusilishwa kwa Lori Lililojaa
Vigogo wa Azimio walipowasilisha rundo la ushahidi katika Mahakama ya Juu. Picha: UGC.
Siku ya Jumatatu, viongozi wa Azimio waliwasili katiak Mahakama ya Upeo wakiwa na rundo la ushahidi lilojaa kwenye lori, ila imewalazimu kupunguza ushahidi huo hadi kurasa 40.
Siku ya Ijumaa, Agosti 26, Fred Orego ambaye ni mmoja wa wakili katika kesi hiyo alisema kupunguzwa kwa stakabadhi za kesi hiyo hadi kurasa 40, inaendana na sheria za mahamakama hiyo.
Azimo Yataka Kesi Zilizowasilishwa na Moses Kuria, Reuben Kigame Kuondolewa Katika Mahakama ya Juu
Kwa mujibu wa sheria za Mahakama ya Upeo, kesi iliyowasilishwa inapaswa kuwa na kurasa zisizozidi 40.
Orego aliongeza kusema kwamba stakabadhi walizowasilisha zinaelezea kwa kifupi maeleoz ya kesi inayosaka kubatilihsa ushindi wa Ruto, na kusema kwamba uchaguzi huo haukuwa huru, wenye usawa na haki.
“Tulichofanya ni kutoa maelezo kwa ufupi, ushahidi uliyowasilishwa hapa na uliobebwa kwa lori siku ya Jumatatu Monday, na kupunguzwa hadi kursa 40 kwa sababu Mahakama ya Upeo ina masharti kali,” Orego alisema.