Baada ya Kumdunda Mandonga Shaban Kaoneka Amtangazia vita Dullah Mbabe

 


Baada ya kumchakaza Bondia Karim Mandonga kwa KO, Bondia Shaban Kaoneka ametangaza rasmi hamu ya kutaka kupambana na Bondia Abdallah Pazzi ‘Dullah Mbabe’.


Kaoneka ambaye anashikilia rekodi ya kumchapa Bondia Hassan Mwakinyo anayetamba Barani Afrika kwa sasa, amesema anaamini muda wa kupamba na Dullah Mbabe umewadia, kwani ana sifda zote za kupanda ulingoni na nguli huyo.


Amesema kwa muda mrefu amekua akipambana na Mabondia wa kawaida (Wasiojielewa), hivyo ni wakati wake sasa kurejesha hadhi kwa kuwachapa Mabondia wanaojielewa kama Dullah Mbabe ambaye hajapanda ulingoni muda mrefu.


“Tambo za Mandonga hazikunitisha, Nilikuwa nafanya mazoezi,Tulivyoanza pambano nilivyomuona nilisema huyu ni wa kupigwa muda wowote”


” Unajua nilishatangaza kustaafu ngumi nilikuwa nataka muda uende ili watu wainjoi kama ningetaka kumpiga round ya kwanza ningeweza. Nilikuwa namtega Kwenye mitego alikuwa anakuja”


“Kama anataka ngumi afanye mazoezi aache maneno. Ngumi haitaki maneno, afanye mazoezi. Ngumi sio kama mpira wa Miguu ukichoka unampasia mwenzio. Ngumi ni wewe mwenyewe”


“Namtaka Dullah Mbabe, uzito wangu na wake ni sawa. Namwambia Dullah atokee promota tukutane. Nimeshachoka kupigana na mabondia wasiojielewa namtaka Dullah”


Kwa mara ya mwisho Dullah Mbabe alipanda ulingoni mwishoni mwa mwaka jana dhidi ya Bondia kutoka DR Congo Erick Tshimanga Katompa, na kupoteza kwa kichapo kikali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad