Balozi wa Marekani Aionya Afrika Kununua Mafuta Kutoka Urusi




Linda Thomas Greenfield akiwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni
BALOZI wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas Greenfield, amesema kuwa Mataifa ya Afrika hayapaswi kununua mafuta kutoka katika nchi ya Urusi.

Akiwa katika mkutano mkuu na waandishi wa habari katika Mji Mkuu wa Uganda Kampala baada ya kumaliza mkutano na Rais Yoweri Museveni, katika mkutano huo Balozi huyo alisema kuwa nchi ya Urusi haijawekewa vikwazo kuuza bidhaa zozote za kilimo.

Lakini Afrika hairuhusiwi kununua mafuta ya Urusi kwa sababu ni kikwazo cha Umoja wa Mataifa na Marekani juu ya nchi hiyo.


Linda Thomas Greenfield amesema Afrika inaweza kununua nafaka kutoka Urusi lakini siyo mafuta
Balozi huyo wakati wa mkutano na Waandishi wa habari alinukuliwa akisema:

“Nchi ikijihusisha na Urusi ambapo kumewekewa vikwazo, basi inavunja vikwazo vyetu vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa, Tunazionya nchi za Afrika zisivunje vikwazo hivyo, ikiwa zitaenda kinyume na kuvunja vikwazo hivyo basi hatua dhidi yake zitachukuliwa”


Linda Thomas Greenfield
Aidha Balozi huyo katika mkutano amesema kuwa Urusi imewekewa vikwazo vya kuuza mafuta yake Afrika, lakini haijazuiliwa kuuza bidhaa zake za kilimo kama vile mbolea pamoja na ngano na nchi za Afrika zinaweza kununua bidhaa hizo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad