Bondia Karim Mandonga leo Jumapili ataenda kuwakata kiu ya burudani mashabiki wake kwenye pambano la kirafiki na Bondia Mussa Omary katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam, kwenye Tamasha la Sensabika (SensaBika Concert).
Lengo la tamasha hilo kubwa lililoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) ni kuhamasisha Watanzania kuhesabiwa, katika zoezi la Sensa linalotarajia kufanyika Jumanne ijayo, Agosti 23.
Aidha, Tamasha la Sensabika linatajwa litaanza saa 12 asubuhi mpaka usiku na kuhusisha michezo mbalimbali, wasanii zaidi ya 50 wanatarajiwa kushiriki Tamasha hilo kubwa ambalo halina kiingilio, wananchi wote wamekaribishwa.