Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema (77) amefariki dunia leo Jumapili, Agosti 21, 2022 alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Jijini Dar es Salaam
Msemaji wa MNH, Aminieli Eligaisha amesema Mrema alilazwa tangu Agosti 16, 2022 na kifo chake kimetokea saa kumi na mbili asubuhi
Enzi za uhai wake, Mwanasiasa huyo Mkongwe aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mgombea Urais wa Tanzania kupitia NCCR-Mageuzi mwaka 1995. Pia, aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR-Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP