Chadema yakerwa na utitiri wa tozo, kodi



Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeeleza kukerwa na hatua ya Serikali kushindwa kutumia rasilimali zilizopo kuongeza vyanzo vya mapato na badala yake inawaminya wananchi kufanikisha hilo.

 Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 28, 2022 na Msemaji wa waliokuwa wagombea ubunge wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, Celestine Simba.

Amesema Serikali ina rasilimali lukuki inazoweza kuzitumia kuongeza mapato yake badala ya kuongeza tozo na kodi mbalimbali, lakini hazitumiki ipasavyo.

"Serikali ina mbuga za wanyama, madini, gesi asilia na vyanzo vyote muhimu vya mapato na ingekuwa makini ingevitumia madhubuti na kuwaondolea wananchi maumivu," amesema.


Endapo vingetumika vema, ameeleza kuwa wananchi wangefurahia mgawanyo wa rasilimali na kuongezewa vipato vyao badala ya kulalamikia maumivu.

Amependekeza kuundwa kwa mbinu na mifumo endelevu ya kukusanya kodi badala ya kubuni vyanzo alivyoviita vya zimamoto.

Hata hivyo, amesema hali hiyo ni matokeo ya udhaifu wa Bunge lililoshindwa kuisimamia Serikali katika matumizi ya rasilimali.


"Bunge na Spika wake (Dk Tulia Ackson) limegeuka kuwa mtetezi wa Serikali, wananchi wanapaswa kutambua kuwa maumivu yote haya yalianzia bungeni kwani walipitishwa mswada wa sheria hii," amesema.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad