Chawa wa Uwoya Amsifia na Apigilia Msumari Kuwa Msipende Kumuiga Mtaumia....


CHAWA WA UWOYA AMSIFIA NA APIGILIA MSUMARI KUWA MSIPENDE KUMUIGA, MTAUMIA...Kwa upande wake, Aristote ni Chawa wa Uwoya ambaye anasema kuwa, kila wanachopenda kumuiga kina madhara yake siku zote hivyo wajifunze au vitu vingine waviangalie tu na kuviacha vipite kama vilivyo.

Aristote nasema kuwa, wapo wengine wanataka kuwa kama alivyo Uwoya ndani ya siku moja, jambo ambalo haliwezekani kwani wakifanya hivyo wataumia.
“Wasijaribu kuiga, wataumia, hawajui mtu amepitia msoto gani mpaka kufikia hapo alipofikia.
“Irene (Uwoya) sasa hivi anahitaji maadui wapya, wale wa zamani wameshakuwa marafiki, wawe wavumilivu wa kila kitu maana wasifikiri kila kitu ni rahisi tu, haiwezekani na siyo kila kitu cha kuiga maana mtu atajikuta anaumia bure,” anasema Aristote akisisitiza watu wamuache Uwoya ainjoi maisha yake.

Tambo hizo za Uwoya zinakuja siku chache baada ya kuwa mwathirika mwingine wa kusambaa kwa picha na video zake za ngono.

Baadhi wafuasi wa Uwoya wanaamini kuwa, pamoja na kuwa na pesa nyingi kiasi cha kuzitapanya kwa starehe za kufuru na kuwamwagia watu, lakini zilishindwa kumnusuru kwenye janga hilo.

Watu wa kada mbalimbali wamekuwa na maoni tofauti huku wengi wakijiuliza kwa nini Uwoya alishindwa kuizima ishu hiyo wakati ana pesa za kutosha na kila siku anajitangaza kuwa ni tajiri wa kutupwa.

Wanajiuliza ameshindwaje kuzuia kuchafuka kiasi hicho ilihali taarifa alikuwa nazo mapema kwamba siku yoyote mzigo utavuja?
Wiki kadhaa zilizopita Uwoya alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kanisa moja mjini Morogoro lililokuwa likiadhimisha miaka minane tangu kuanza kutoa huduma.

Pia Uwoya alikuwa mgeni rasmi wa kuzungumza na kikundi cha kina mama kanisani hapo.

Wengi baada ya kuona hivyo waliamini kwamba Uwoya mwisho wa siku ameupokea wokovu na kuacha mambo ya hovyo ila ndiyo tena sasa limempata baya zaidi la kuchafua jina lake kabisa @ireneuwoya8

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad