Diamond Adaiwa Kumharibu Zuchu, Azua Gumzo Nchini Afrika Kusini




Diamond na Zuchu wamekuwa kwenye mahusiano ambayo hayajawekwa wazi kama ni wapenzi au ni mtu na Bosi wake
ZUCHU; ni msanii wa moto ile mbaya kunako lebo kubwa kabisa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambaye anazidi kuwa gumzo kutokana na tetesi za mahusiano baina yake na bosi wake, Diamond Platnumz ambaye anadaiwa kumharibu mrembo huyo.

Diamond anadaiwa kumfundisha Zuchu maisha ya kufeki baada ya mrembo huyo kuposti picha zake akiwa amemuiga katika mitindo yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zuchu ameposti picha na video akionesha jinsi ambavyo amemuiga Diamond kwa kuweka urembo katika meno yake pamoja na pete za kimapambo; pete moja kubwa kwenye kidole cha mwisho cha mkono wa kulia, kama ambavyo Diamond anavaa.

Akiwa nchini Afrika Kusini akiandaa video mpya, Zuchu amezua gumzo kama lote kutokana na uigaji huo kwa bosi wake na kufanya wengi waamini kwamba wawili hao wapo kwenye mahusiano; uvumi ambao umekuwa ukizungumziwa zaidi kwa muda mrefu sasa.


 
“Hapa sasa ni tabasamu zuri tu. Ahsante sana Diamond Platnumz,” anasema Zuchu akifuatisha na picha hizo na maneno hayo yaliyoonekana kwamba anamshukuru bosi wake kwa kumfunza mbinu hizo za kujiremba ambazo kwa muda mrefu zimekuwa ni za Diamond tu mpaka kuwa kama nembo ya utambulisho wake.


Zuchu na Diamond wote ni mastaa waliopo kwenye Lebo ya WCB
Sasa, waja kama kawaida yao, wamezuka kwenye picha hizo alizozipakia Zuchu na kuachia yao ya moyoni ambapo walisema sasa huo ni uthibitisho tosha kwamba wawili hao wamepanga kuigana hadi uvaaji maana wao ni mwili mmoja kimtindo.

Zuchu na Diamond kwa muda mrefu wamekuwa wakisemwa kuwa wapo katika mahusiano japokuwa hakuna hata mmoja baina yao amekiri wazi wala kukataa bayana uwepo wa mahusiano yao.


Zuchu akiwa amevaa Pete kama ya Diamond Platnumz
Zuchu amekuwa akibanwa sana katika mahojiano kwa maswali ya uwepo wa mahusiano yao, lakini amekuwa akiguna na kumalizia kwamba anamchukulia Diamond kama bosi wake kimuziki.

Kwa upande wake, Diamond amekuwa akiulizwa ambapo wakati mmoja wakiwa kwenye mahojiano na pamoja na Zuchu, mwanadada huyo aliulizwa swali la kuchumbiana na Diamond, lakini Simba akadakia kwa haraka na kumkatiza huku akisema kwamba maswali kama hayo yana ukakasi na ndiyo maana alimsaidia Zuchu kujibu ili asije akazungumza mambo yasiyofaa.


Staili ya meno ameweka kama Diamond Platnumz
Familia nzima ya WCB imekuwa ikilikwepa suala hilo ambalo mpaka sasa chawa wa Diamond, Baba Levo pekee ndiye anaonekana kuzungumza tena kwa kunadi kwamba Diamond au Mondi na Zuchu ni wapenzi japo maneno yake yanachukuliwa kimzaha.
Cc; @sifaelpaul

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad