Supastaa @diamondplatnumz kwenye mahojiano yake jana Alhamisi, Agosti 11 katika kipindi cha #TheTouchDown cha radio ya nchini Afrika Kusini iitwayo Metro FM kwa mara ya kwanza ameweka wazi juu ya Helikopta yake aliyonunua na kukazia kuwa usafiri wake huo una uwezo wa kuruka usiku.
Diamond amesema, Helikopta hiyo aliyonunua ndio ya kwanza kati ya Helikopta chache Afrika Mashariki zenye uwezo wa kuruka usiku kwani Helikopta nyingi zinaruka mwisho SAA 12 jioni.
"Nilinunua kwanza ndege, jana nimetoka kununua Helikopta, na baada ya wiki NNE itakuwa tayari imekuja Tanzania. Na Helikopta yangu ni kati ya Helikopta chache Afrika Mashariki zenye uwezo wa kuruka usiku yaani baada ya jioni SAA 12." - ameeleza @diamondplatnumz
Kwa msaada wa mtandao juu ya kufahamu undani zaidi wa Helikopta, inaelezwa kwamba... Helikopta nyingi huwa haziruki usiku kutokana na kuwa zinaruka umbali wa chini tofauti na ndege hivyo kuhatarisha maisha ya waliopanda. Helikopta haishauriwi iruke usiku kwa sababu inaweza ikagonga mwamba, mti mkubwa n.k tofauti na ndege ambayo inakuwa juu sana.
Aidha, kwenye maelezo mtandaoni, Helikopta zinazotajwa kuwa zina uwezo wa kuruka usiku ni zile za Kijeshi, ama za huduma (msaada kiafya, moto n.k) ambapo zinakuwa na vifaa mahususi kwa ajili ya kuona usiku. Hivyo @diamondplatnumz Helikopta yake amesema ni moja kati ya ambazo zina huo uwezo wa kuruka usiku.