Ewura Watangaza Bei Mpya ya Mafuta Mwezi August


Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini, bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, August 03, 2022.

EWURA imesema “Bei za Mafuta katika soko la dunia zimeendelea kuongezeka na kusababisha bei za mafuta katika soko la ndani kuongezeka pia. Ili kupunguza madhara ya ongezeko hilo katika soko la ndani, Serikali imetoa ruzuku ya bilioni 100 kwa ajili ya bei za mafuta hapa nchini kwa Agosti 2022, Serikali kwa kutoa ruzuku hiyo, imepunguza bei za bidhaa za mafuta kwa Agosti 2022”

Bei za mafuta za rejareja kuanzia kesho Agosti 3, 2022, kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Petroli itauzwa shilingi 3,410, Dizeli 3,322 na mafuta ya taa yatauzwa kwa shilingi 3,765, Tanga Petroli itauzwa 3,435 na Dizeli itauzwa 3,349.

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne Agosti 2, 2022 na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na kusema petroli mkoani Mtwara itauzwa 3,393kwa lita na dizeli itauzwa 3,351 kwa lita, aidha bei ya petroli kwa Arusha ni 3,492 kwa lita na dizeli ni shilingi 3,406.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad