Fomu 34A Zapatikana Tupu Katika Kituo cha Kupigia Kura cha Shule ya Msingi ya Majengo
Maafisa wanaosimamia zoezi la kuhesabu tena kura za urais katika vituo 15 vya kupigia kura. Picha: UGC.
Wakati wa shughuli hiyo iliyofanyika Jumatano, Agosti 31, maafisa wanaosimamia zoezi hilo waligundua fomu 34A katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi ya Majengo, Mombasa ni tupu.
Maafisa hao walisema idadi ya kura zilizopigwa kwa kila mwaniaji hazikuandikwa kwenye fomu hiyo, pamoja na kura zilizoharibika.
Baada ya kusesabu tena, ilibainika kwamba kiongozi wa Azimio la Umoja Raila Odinga, alipata kura 139 dhidi ya William Ruto aliyeapata kura 83.
Kioni: Maafisa wa IEBC Waliovaa Barakoa Walifanyia Kampeni UDA Kwenye Vituo vya Kupigia Kura
Vile vile ndani ya sanduku za kura, kulipatikana kura moja ya mwakilishi wadi (MCA).
Hata hivyo, TUKO.co.ke imebaini kwamba matokeo hayo ni sambamba na yale yaliyopakiwa kwenye mtandao rasmi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).
Kama ilivyoripotiwa awali, Mahakama ya Juu ilitoa agizo kwa IEBC kuwasilisha masanduku ya kura ili yakaguliwe tena, kwenye kesi ya kupinga ushindi wa Ruto.
Vituo hivyo ni pamoja na he Shule za Msingi za Nandi Hills na Sinendeti katika Kaunti ya Nandi, Shule za Msingi za Belgut, Kapsuser na Chepkutum katika Kaunti ya Kericho, Jomvu, Mikindani na Ministry of Water Tanks, Kaunti ya Mombasa.
Zingine ni Shule za msingi za Mvita, Majengo na Mvita, Kaunti ya Mombasa, Tinderet, Kaunti ya Nandi, Jarok, Gathanji na Kiheo, Kaunti ya Nyandarua.
Mahakama ya Juu: Mawakili wa Raila Wadai Kura Zake Zilimegwa na Kuongezewa Ruto