Gari ya Princess Diana yauzwa bil1.7/- mnadani



GARI maarufu ya kifamilia katika miaka ya 80 iliyokuwa ikitumiwa na Princess Diana wa Uingereza imeuzwa kwa zaidi ya Sh bilioni 1.79 (karibu dola za marekani 764,000) kwenye mnada na kuweka rekodi ya mauzo kwa gari kama hilo kuwahi kuuzwa kwenye mnada.

Diana aliendesha Ford Escort RS Turbo nyeusi ya mwaka 1985 kwa karibu miaka mitatu na alipigwa picha mara kadhaa akiitumia kwenye safari za maduka ya kifahari ya London ya Chelsea na Kensington.

“Huu ni wakati mdogo wa historia, mabibi na mabwana,” dalali alisema alipoanza zabuni kwa pauni 100,000 ($ 117,000) – kiasi ambacho ni zaidi ya gari kama hilo, rangi nyeupe, lililopigwa mnada mwaka jana. 

Bei ya mwisho ya mauzo ya gari la Diana, ikijumuisha malipo ya asilimia 12.5 ya mnunuzi, ilikuwa zaidi ya Sh bilioni 1.99 ($850,000).


Princess Diana alifariki miaka 25 iliyopita lakini anatajwa kama mfano wa kuigwa kwa wanawake

Uuzaji huo ulikuja siku chache kabla ya kumbukumbu ya miaka 25 ya ajali ya gari huko Paris ambayo ilimuua Diana na mpenzi wake, Dodi Fayed. Diana hakuwa akiendesha gari hilo – Mercedes-Benz S-280 – wakati lilipo anguka kwa mwendo kasi mapema Agosti 31, 1997.

Mwaka jana, kipande cha keki kutoka katika harusi yake ya kifalme na Prince Charles – chenye zaidi ya miaka 40 sasa, ingawa hakifai kwa chakula – kilipigwa mnada nakuuzwa Sh milioni 4.6 (karibu $2,000).

Wale waliohudhuria mnada wa Jumamosi hakika walionekana kuwa na shauku ya kuhifadhi kipande cha historia ya Uingereza na ukumbusho kwa “Mwanamfalme.” 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad