Geita Gold Waiiga Simba Kimataifa..Nao Wakimbilia Kule Kule Wanapochotaga Mastaa wa Maana

 


Timu ya Geita Gold Fc leo imetangaza kumsajili Shawn Oduro raia wa Ghana kama sehemu ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi Kuu na mashindano ya kimataifa.

Huu ni usajili wa nne kutangazwa na timu hiyo baada ya George Wawa kutoka Dodoma Jiji FC, Hussein Kazi (Polisi Tanzania) na Kipa Arakaza MacAthur kutoka Burundi huku ukiwa usajili wa pili wa kimataifa.


Nyota huyo amemtambulishwa kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii baada ya kusaini kandarasi ya miaka miwili huku akitazamiwa kuongeza nguvu kwenye eneo la ulinzi na kuziba pengo lililoachwa na beki mkongwe, Juma Nyosso aliyetimkia Ihefu ya jijini Mbeya.


"Geita Gold FC tunayo furaha kuwataarifu kuwa tumeingia mkataba wa miaka miwili na mlinzi wa kati Shown Oduro kutoka Acra Ghana,"


"Uduro anakuja kuongeza idara ya ulinzi kuhakikisha ukuta unakuwa salama," imesema taarifa ya klabu hiyo.


Usajili huo ni kama Geita Gold imejibu mapigo kwa Simba iliyomshusha mchezaji kutoka Ghana, Agustine Okrah.


Ofisa Habari wa Geita Gold, Samwel Dida amesema kuwa wamejipanga vyema kuimarisha kikosi chao na kuandaa kikosi tayari kwa msimu ujao wa ligi na mashindano ya kimataifa.


“Tupo tayari kuandaa vijana wetu tayari kwa mapambano ya msimu ujao na tutaendelea kushusha vifaa vingine vya ndani na nje ya nchi tayari kwa mashindano yote msimu ujao” amesema Dida.


Geita Gold inatarajiwa kufungua pazia la ligi kuu kwa kuwavaa Simba SC mchezo wa kwanza wa Ligi msimu huu utakaopigwa Agosti 17 uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam huku wapinzani wao hao wakiwa na nyota Augustine Okrah raia wa Ghana aliyetua msimu huu. 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad