Shangwe, nderemo na vifijo vya mapokezi yake aliporejea @krcgenkofficial ni uthibitisho tosha wa ubora mkubwa alionao na namna wapenzi wa soka wa Ubelgiji wanavyothamini mchango wake.
Mbwana Samatta sio tu anaipeperusha bendera ya Tanzania Ubelgiji na Ulaya yote bali kwa ukubwa zaidi anawavutia vijana wengi kushiriki soka kwa kuweka juhudi na maarifa zaidi. Leo ukienda viwanjani Tanzania unaona vipaji lukuki tena kutoka kwa vijana wenye ndoto kubwa, na sio tu kuleta heshima ya mtaani tu au kuzawadiwa vitu vidogovidogo.
Wanafuata nyayo za @samagoal77
NB. Miaka 10 ijayo naziona ligi kubwa duniani zikiwa na Wachezaji wengi wa Tanzania kutokana na jinsi vijana walivyodhamiria kufika mbali, wadau wanavyoitikia kuwekeza kwenye mpira na Serikali ilivyoweka dhamira ya kunyanyua sekta ya kichezo kimkakati.
Michezo ni furaha, biashara, afya na utambulisho wa Taifa.