Moja kati ya washambuliaji mahiri kwa sasa katika Ligi Kuu ya England ni staa wa kimataifa wa Norway Earling Haaland (22) Kutokana na uhodari wake wa kupachika nyavu toka wakati huo akiwa Borussia Dortmund, Haaland ameanzia alipoishia kwa maana toka ajiunga na Man City ameonesha ubora ule ule aliokuwa nao Dortmund.
Kwenye mchezo wa Ligi Kuu England wa Man City dhidi ya Crystal Palace uliyochezwa katika uwanja wa Etihad leo na kumalizika kwa Man City kupata ushindi wa 4-2 wakitokea nyuma, baada ya dakika 45 za kwanza kwenda mapumziko wakiwa nyuma 2-0, Haaland alikuwa mkombozi wa game hiyo kwani baada ya Bernardo Silva kufunga goli la utangulizi dakika ya 53, Haaland alipiga hat-trick kwa kufunga magoli matatu dakika ya 62, 70 na 81.
Hiyo ilikuwa ni kufuta machungu yaliotangulia kwa beki wao John Stones kujifunga dakika ya 4 ya mchezo na Andersen kufunga la pili kwa Crystal Palace dakika ya 21, Haaland akiwa na umri wa miaka 22 tu tayari anakuwa na idadi kubwa ya hat-trick 13 kuliko baadhi ya wachezaji wakubwa katika soka kama Wayne Rooney mwenye hat-trick 10, Samuel Eto’o 9 na Fernando Torres 8.
Katika hat-trick 13 za Haaland alizowahi kufunga leo ndio kafunga ya kwanza akiwa England, moja alifunga akiwa na Molde, Salzburg 5, Borussia Dortmunda 4 na mbili akiwa na timu yake ya Taifa ya Norway.