msemaji wa klabu ya Yanga Haji Sunday Manara usiku wa jana ameamua kumuuomba msamaha waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa.
Manara kupitia mitandao yake ya kijamii amepost clip ikimuonyesha akimuomba Waziri msamaha kutokana na sababu aliyoieleza.
Ikumbukwe Manara amefungiwa na TFF miaka miwili na kupigwa faini ya milioni 20 kutokana na maneno mabaya aliyomtolewa rais wa TFF Waleci Karia ikiwemo matusi.
Manara wakati akizungumza baada ya hukumu yake alimshutumu Waziri mwenye dhamana ikiwemo kuwatuma TFF kuwa wampe adhabu hiyo.