Hamisa Mobetto " Baba Yanga Hakuwahi Kuwa na Instagram, Diamond Kuto Post Haiongezi Wala Kupunguza Chochote




Kupitia Amplifaya ya Clouds Fm, Mrembo na mwanamitindo Hamisa Mobetto amejibu sababu za kwanini mzazi mwenzie, Diamond Platnumz hakumpost mtoto wao, Dylan kivyovyote vile siku ya birthday yake August 08 mwaka huu. Hamisa amedai hajui sababu ni nini, uwenda hilo swali angeulizwa Diamond mwenyewe. Hamisa pia ameeleza kuwa Baba yake hakuwahi kuwa na Instagram, hivyo Hamisa hakuwahi postiwa na haikuongeza wala kupunguza kitu mbali na ilivyotakiwa.


Kuhusu kama bado Msanii huyo (Diamond) anaendelea kutoa matunzo kwa mtoto wake, Hamisa hakutaka kuweka wazi ishu hiyo. Ikumbukwe tu baada ya Diamond kutoshare kwa namna yoyote ile birthday ya mtoto wake August 08 mwaka huu, Mama mzazi wa Dylan, Hamisa Mobetto alimfuta Diamond kwenye Bio ya Instagram page ya Dylan.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad