Hatimaye Diamond Platnumz Ameijibu Barua ya Wazi ya Romy Jons "Wasanii Hawana Shukrani"


Hatimaye @diamondplatnumz ameijibu ile post iliyoitwa barua ya wazi kutoka kwa Kaka yake ambaye pia ni DJ wake @romyjons ambapo usiku wa kuamkia leo alimwandikia Diamond akimshauri aachane na shughuli ya kusaidia wasanii kutokana na matokeo mabaya ambayo amekuwa akiyapata kwa wasanii hao baada ya kufanikiwa.


Romy kwenye maelezo yake amemtaka mdogo wake Diamond ajikite tu kwenye biashara zake akihoji, "Kwanini usiwekeze nguvu, akili, pesa kwenye biashara yako ya radio na tv?" - alihoji @romyjons


Diamond ameamua kuijibu post hiyo kupitia sehemu ya komenti ambapo ameeleza kwamba; Kiwanda cha muziki nchini hakina shukrani, akiwatolea mfano wasanii wa Nigeria, Wizkid na Davido ambao amegundua kwanini hawakujikita kwenye kusaidia wasanii chipukizi waliowasaini.


Kwenye maelezo ya mwisho katika ujumbe wa Diamond, ameeleza ikiwa hii nchi ni yetu hivyo ni jukumu lake kuendelea kunyanyua vipaji toka mtaani ili nao wajikomboe Kimaisha.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad