Hatimaye Msanii Aslay Ametangaza Rasmi Kujiunga na Lebo kubwa Afrika ya Rockstar


Hatimaye msanii @aslayisihaka ametangaza rasmi kujiunga na lebo kubwa Afrika ya Rockstar ambapo ameeleza amejiunga hivi karibuni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Aslay ambaye amewahi kutamba na hits nyingi ndani na nje ya nchi, ameandika..

"Ninafuraha kuwaambia Mashabiki, Vyombo vya habari na kila anayenifuatilia kwamba hivi karibuni nimejiunga na RockStar Africa @rockstarafrica. Imekuwa safari ndefu yenye matumaini makubwa katika kusimamia kazi zangu za muziki. Hivyo basi, Nawaarifu kutegemea mengi makubwa katika muziki wangu na kuniona katika hatua kubwa zaidi.

Nina kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kipindi chote ambacho nilikuwa kimya, hakika nimejifunza Mengi🙏🏽. Ningependa kuchukua wakati huu Pia kutoa shukrani zangu kwa kila mmoja wenu kwa support mnayoendelea kunipa katika muziki wangu hata wakati nilipokuwa kimya. Asanteni sana🙏🏽❤️" - unasomeka ujumbe wa @aslayisihaka

Umeikumbuka ladha ya muziki mzuri toka kwa Aslay? andaa masikio yako.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad