Hatimaye namba ‘D’ iliyokuwa ikitumika kwa usajili wa magari hapa nchini Tanzania yafikia mwisho na hivyo kuruhusu namba mpya ‘E’ kuanza kutumika rasmi kwa ajili ya usajili wa magari mapya hapa nchini Tanzania.
Itakumbukwa kwamba namba ‘D’ ndiyo namba ambayo imeweka rekodi ya kutumika kwa muda mrefu Zaidi kwa ajili ya usajili wa magari hapa nchini ukilinganisha na namba nyingine kama ‘A’, ‘B’, ‘C’. ambazo zilitumika kwa muda mfupi, ambapo inakadiriwa kwamba namba D imekuwa ikitumika kwa Zaidi ya miaka 6 tangu ilipoanza kutumika mwaka 2014.
Kutumika kwa namna ‘D’ kwa muda muda mrefu kulisababishwa na kupungua kwa kasi ya uagizaji wa magari mpaka pale ilipofikia mwezi Machi, 2021 ambapo ongezeko kubwa la uagizaji wa magari kutoka nje ya nchi ulishuhudiwa na hivyo kupelekea namba ‘D’ kuanza kutumika kwa kasi hadi kufikia mwisho wake wa matumizi.
Nini, mtazamo wako kuhusiana na jambo hili?