Hivi ndivyo Ulimwengu wa siri wa kutumiana picha za utupu za wanawake mtandaoni bila ridhaa yao unavyoshamiri duniani



Maelfu ya wanawake wanakabiliwa na vitisho na ulaghai kutoka kwa watu wasiojulikana baada ya maelezo yao ya binafsi, picha zao za faragha na video walizochapisha kwenye jukwaa la mtandao wa kijamii wa Reddit.

BBC imefichua mtu aliyekuwa nyuma ya moja ya vikundi hivi.

"$6 kwa picha zake za utupu, nitumie ujumbe DM."

"Nina video zake ambazo ninataka kuuza."

"Tutamfanya nini?"

Kuangalia picha na maoni mtandaoni kumeniacha mgonjwa.

Kulikuwa na maelfu ya picha. Utiririshaji wa picha za wanawake walio watupu bila nguo au waliovalia kiasi unaoonekana kutokuwa na mwisho. Chini yake, wanaume hao walichapisha maoni mabaya, ikiwa ni pamoja na vitisho vya ubakaji. Mengi yalikuwa maoni machafu kutumwa hapo.

Kidokezo kutoka kwa rafiki yangu kilimuongoza kwenye picha hizi. Moja ya picha zake zilichukuliwa kutoka Instagram na kuwekwa kwenye Reddit.

Hakuwa uchi, lakini hata hivyo, iliwekwa pamoja na lugha ya ngono na ya kudhalilisha.

Nilichopata ni soko. Mamia ya watu ambao hawakujulikana walijitolea kutumiana, kubadilishana na kuuza picha chafu na kila kitu kilionekana kuwa kilitoka bila idhini ya wanawake waliopigwa picha.

Ilikuwa kama mageuzi mapya ya kile kinachoitwa ponografia ya kulipiza kisasi, ambapo mambo binafsi ya faragha huwekwa mtandaoni bila idhini, kwa kawaida na washirika wa zamani wenye hasira za kuachana

Sio tu kwamba picha hizi za faragha zilitumwa miongoni mwa maelfu ya hadhira, lakini wanaume, waliojificha nyuma ya kivuli cha kutokujulikana, waliunganishwa pamoja ili kufichua utambulisho halisi wa wanawake hawa, zoezi linalojulikana kwa Kiingereza kama doxing. Anwani zao, nambari za simu, na majina ya kwenye mitandao ya kijamii walipeana mtandaoni na wanawake hawa baadaye walilengwa na maoni machafu ya kingono, vitisho na ulaghai. Nilihisi kama nilikuwa nimejikwaa kwenye kona yenye giza sana ya mtandao, lakini yote haya yalikuwa yakifanyika kwenye jukwaa kubwa la mitandao ya kijamii.

Historia yenye utata
Inajielezea kama "ukurasa wa mbele wa mtandao". Ina hadhira ya takriban watumiaji milioni 50 kila siku duniani kote kwa kuwaruhusu watu waanzishe na kudhibiti mijadala, Reddit katika kipengele kinachojulikana kama "subreddits,". Subreddits nyingi hazina madhara, lakini Reddit ina historia ya kukaribisha maudhui ya ngono yenye utata.

Mnamo mwaka wa 2014, idadi kubwa ya picha za binafsi za watu mashuhuri zilitumwa kwenye wavuti, na miaka minne baadaye, Reddit ilifunga kikundi kilichotumia teknolojia ya "deepfake", aina ya akili ya bandia ili kuweka juu picha ya watu mashuhuri kwenye video za ngono.

Ili kukabiliana na mizozo hii, kampuni hiyo yenye makao yake makuu nchini Marekani ilianzisha sheria kali zaidi na ikaimarisha marufuku yake ya kuchapisha au kutishia kuchapisha maudhui ya kingono au ya fargha kutoka kwa watu bila ridhaa yao.

Nilitaka kuelewa jinsi picha za fargha za wanawake zilivyoendelea kutumwa kwenye Reddit na ni athari gani walipata wanawake walioathiriwa.

Kisha nilitaka kujua ni nani alikuwa nyuma ya haya yote.

Marufuku ya Reddit haikufanya kazi.

Kulikuwa na dazeni za subreddits zilizojitolea kutuma picha za faragha za wanawake kutoka kote Uingereza.

Ya kwanza ililenga wanawake wa Asia Kusini na ilikuwa na watumiaji zaidi ya 20,000, ambao wengi wao walionekana kuwa wanaume kutoka jamii moja na kuna maoni ya Kiingereza, Kihindi, Kiurdu na Kipunjabi.

Niliwatambua baadhi ya wanawake kwa sababu walikuwa na wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii. Baadhi hata mimi binafsi niliwajua.

ggg
Maelezo ya picha, Watumiaji wasiojulikana walituma picha za wanawake bila ruhusa na maoni ya udhalilishaji kuwahusu na vitisho.
Mwanamke mmoja tuliyewasiliana naye anasema sasa anapokea jumbe za ngono kwenye mitandao yake ya kijamii "kila siku", baada ya kundi hilo kuchapisha picha yake akiwa na blauzi iliyofunika kifuani tu kwenye Instagram sambamba na maoni kuhusu kumbaka.

Wanaume kwenye subreddit pia walikuwa wakituma na kuuza picha za uchi za wanawake. Picha hizi zilionekana kama selfie ambazo zilitumwa kati ya wapenzi wao na hazikukusudiwa kutumiwa na umma.

Pia kulikuwa na video ambazo ilionekana kuwa wanawake hao walikuwa wamerekodiwa kwa siri wakati wa tendo la ndoa.

"Nitakutafuta"
Ujumbe mmoja ulikuwa na picha za mwanamke aliye uchi akifanya ngono ya mdomo.

"Je, kuna mtu yeyote aliye na video ya hii?" mtumiaji asiyejulikana aliuliza,

"Nina jalada lake lote kwa $ 6," mwingine alijibu.

"Mitandao yao ikoje?" aliuliza wa tatu.

Ayesha - sio jina lake halisi - aligundua video zake zikitumwa kwenye subreddit mwaka jana. Anaamini kuwa mpenzi wake wa zamani alimpiga picha kwa siri.

Sio tu kwamba ilibidi ashughulikie uaminifu wake ukivunjwa, lakini pia alilazimika kukumbana na wimbi la unyanyasaji na vitisho kwenye mitandao ya kijamii wakati maelezo yake ya kibinafsi yalipowekwa kwenye jukwaa hilo.

"Usipofanya mapenzi na mimi, nitawatumia wazazi wako. Nitakuja kukuchukua... Usipokubali kufanya mapenzi na mimi, nitakubaka." Wanaomfuatilia pia walijaribu kumtusi ili kupata picha zake zaidi.

"Mimi ni Mpakistani, na si sawa katika jamii yetu kufanya mapenzi kabla ya ndoa au kitu kama hicho, hilo halikubaliki," anasema.

Aisha aliacha kujumuika au hata kuondoka nyumbani na hatimaye akajaribu kujiua. Baada ya jaribio lake la kujiua, ilimbidi kuwaambia wazazi wake kilichotokea. Mama yake na baba yake waliingia kwenye msongo wa mawazo, anasema. "Niliona aibu sana kwa kila kitu kilichokuwa kikiendelea na kuwaweka katika hali hii," aeleza. Aisha aliwasiliana na Reddit mara kadhaa. Kuna muda, video iliondolewa mara moja, lakini ilichukua miezi minne kuondoa nyingine.

Na hakuishia hapo. Maudhui yaliyoondolewa tayari yalikuwa yametumwa kwenye tovuti nyingine za mitandao ya kijamii, hatimaye kuonekana tena kwenye subreddit ya awali mwezi mmoja baadaye.

"Mkusanyaji"
Sehemu ndogo iliyomwaibisha na kumnyanyasa Aisha iliundwa na kusimamiwa na mtumiaji anayeitwa Zippomad, jina ambalo hatimaye lingetoa fununu ya mahali alipokuwa.

ggg
Maelezo ya picha, Watumiaji wa majukwaa haya walituma maelezo binafsi ya wanawake hawa ili kuwapata katika maisha halisi.
Kama msimamizi, Zippomad alitakiwa kuhakikisha kuwa kikundi chake cha majadiliano ya subreddit kinafuata sheria za Reddit. Lakini alifanya kinyume.

Tangu BBC ilipoanza kumfuatilia kwa mara ya kwanza ameunda akaunti mpya mara tatu, baada ya jina la awali kufungwa na Reddit kwa sababu ya malalamiko.

Kila akaunti mpya alitumia tofauti ya jina moja, ikiwa ni pamoja na matusi ambayo yanakera sana kurudiwa. Kila moja ilikuwa na maelfu ya watumiaji.

Biashara ya picha za utupu imeenea kiasi kwamba wataalam wa unyanyasaji mtandaoni wanaipa jina: utamaduni wa mkusanyaji. Clare McGlynn, profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha Durham nchini Uingereza na mtaalamu wa aina hii ya unyanyasaji mtandaoni, anasema: "Hili sio jambo la wapotoshaji au wa ajabu wanaofanya hivi. Kuna wengi na kuna makumi ya maelfu ya wanaume".

Anasema kuwa wanaume wengi wanaohusika hupata hadhi katika jamii hizi kwa kukusanya mikusanyiko mikubwa ya picha bila idhini. Uhifadhi huu wa kupita kiasi unaweza kufanya iwe vigumu kuondoa, kama Ayesha aligundua wakati video zilizoondolewa zilichapishwa tena kutoka kwa mikusanyiko mingine. Wanawake saba ambao walijaribu kuondoa picha zao kutoka Reddit waliniambia hawakuhisi kampuni hiyo ilikuwa ikifanya vya kutosha kusaidia.

Reddit ilituambia kwamba iliondoa zaidi ya picha 88,000 za ngono zisizo na ridhaa mwaka jana na inasema inalichukulia suala hilo "kwa uzito mkubwa."

Inasema hutumia zana za kiotomatiki za moja kwa moja na ina wafanyikazi waliojitolea kutafuta na kuondoa picha za faragha zilizochapishwa bila ruhusa.

"Tunajua tuna kazi zaidi ya kufanya ili kuzuia, kugundua na kuchukua hatua kwa yaliyomo kwa haraka na kwa usahihi zaidi, na sasa tunawekeza katika timu zetu, zana na michakato ili kufikia lengo hili," msemaji wa kampuni alisema.

Mwanya halali
Kama makampuni ya teknolojia, sheria ya Uingereza inapigania kuwalinda wanawake dhidi ya kutumwa picha zao za binafsi mtandaoni.

ggg
Maelezo ya picha, Georgie anasema kwamba kwa sababu ya pengo katika sheria, mpenzi wake wa zamani hakuweza kufunguliwa mashtaka baada ya kutuma picha zake wazi.
Mtu asiyemfahamu alipowasiliana na Georgie na kumwambia kwamba picha zake chafu zilikuwa zimetumwa mtandaoni, alienda polisi. Alijua kwamba mtu mmoja tu ndiye angepaswa kuzifikia.

"Siwezi hata kuhesabu ni watu wangapi wanaweza kuwa wameona tayari. Na hakuna njia ya kuwazuia watu zaidi kuona," anasema.

Mpenzi wake wa zamani alimtumia ujumbe mfupi akikiri kwamba alituma picha hizo, lakini anasema alimwambia "hakuwa na nia ya kuniumiza au kuniaibisha."

Kuwajibika
Alitaka kumfuatilia Zippomad, mtumiaji wa Reddit aliyeunda jukwaa lililolenga wanawake wa Asia Kusini, akiwemo Ayesha. Nilipoangalia historia yake kwenye tovuti, hakukuwa na majina halisi, anwani za barua pepe au picha.

Jina lake la mtumiaji pekee ndilo lililotoa kidokezo kwa yeye ni nani, kwa hiyo niliwasiliana naye kwa kutumia akaunti fake na kujitolea kuinunua.

Alikubali kukutana na mwandishi wetu wa siri hatimaye alikutana uso kwa uso na mwanamume aliyeunda jukwaa hilo ambapo faragha nyingi za wanawake zilikuwa zimekiukwa.

Jina lake ni Himesh Shingadia. Ana elimu ya chuo kikuu na anafanya kazi kama meneja katika kampuni kubwa. Hakutarajia angepatikana hata kidogo.

ggg
Maelezo ya picha, Himesh Shingadia anasema aliunda jukwa kwenye Reddit "kuthamini wanawake wa Asia Kusini."
Baada ya kuwasiliana na kipindi cha Panorama cha BBC, Shingadia alifuta subreddit yake. Katika taarifa, anasema kundi hilo lilinuia "kuthamini wanawake wa Asia Kusini." Kutokana na wingi wa watumiaji, anasema aligundua haiwezi kusimamia kongamano hilo.

Anasema hakuwahi kutuma maelezo ya faragha ya mtu yeyote au kufanya biashara ya picha mwenyewe na anasema alisaidia kuondoa maudhui ya ngono alipoulizwa na wanawake.

"Zippomad anaona aibu sana kwa matendo yake, hii haionyeshi utu wake halisi," taarifa hiyo ilisoma.

Reddit pia iliondoa vikundi vingine kama hivyo

Hiyo ina maana kwamba karibu picha za wanawake elfu moja hatimaye zimeeondolewa lakini hiyo ni faraja kubwa baada ya maumivu ya kufichuliwa bila ridhaa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad