IEBC, kupitia kwa afisa wake Kamishna Justus Nyangaya, imesisistiza kuwa hakuna mgombea yeyote wa urais ambaye aliongezewa kura zisizokuwa zake.
“Waliandika 14,760 katika fomu B. Na katika fomu C ibadibilishwa na kurejesha kuwa 14,860. Ruto William ana 41,050. Hakuna mahali ambapo tuliongeza 10,000 kwa mgombea yeyote. Natumahi hili limeeleweka na litarekebishwa. Asante,” Nyangaya alisema.
Kwa mujibu wa ripoti ya IEBC, Ruto alikuwa ameorodheshwa kupata kura 51050 katika eneo bunge la Kiambu katika Fomu 34B badala ya 41050.
Ni kosa mabalo lilitambuliwa wakati wa kujumuishwa kwa kura na likarekebsishwa mara moja.
Hali ya kujumusiha kura inaendelea katika ukumbi huo wa Bomas ambapo maajenti wa Azimio na Kenya Kwanza wamekodoa macho kweli kweli.
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati ameambia kituo cha habari cha Reuters kwamba maafisa wake wamewekwa kwenye kona na mawakala wa wawaniaji wa kisiasa.
"Hali hapa imekuwa ni kama ukaguzi wa kimahakama," Chebukati aliambia waandishi wa Reuters.