Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungulia mashtaka ya kimaadili Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said na aliyekuwa Ofisa wa Klabu hiyo Haji Manara “Kamati ya Maadili ilimfungia miaka miwili Manara kujihusisha na shughuli yoyote ya mpira wa miguu lakini ameshindwa kutekeleza adhabu hiyo”.
Kamati imesema Injinia Hersi amefunguliwa mashtaka kwa kwenda kinyume na ibara ya 16(1) (a) ya Katiba ya TFF pamoja na ibara ya 1(6) ya Katiba ya Yanga.
Baada ya Manara kuadhibiwa na kamati ya Maadili ya Sekretarieti barua Hersi kuhakikisha klabu yake inaheshimu uamuzi huo
Mwenyekiti wa kamayi ya maadili tayari amepelekewa mashtaka hayo na walalamikiwa watapewa mashtaka na mwito mara baada ya kamati kupanga kusikiliza mashtaka hayo.
Jana kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi Haji Manara alitambulisha wachezaji wa Yanga.