Irene Paul "Kuna Muda Natamani Ndoa"


Muigizaji mahiri wa filamu nchini, ambaye kwasasa anafanya vizuri kupitia tamthilia mbalimbali ikiwemo Juakali, @irenepaul001 amesema anatamani ndoa ila akikumbuka matukio hamu inamuisha.

Irene ambaye ni mshindi wa tuzo ya muigizaji bora wa kike mwaka 2015 (Tanzania Films Awards), ni mama wa mtoto mmoja wakike na alifunga ndoa mwezi Machi, mwaka 2017.

Aidha, ametoa kauli ya kuna muda anatamani ndoa kupitia ukurasa wake wa Instagram akieleza kwa ufupi amejiwazia tu. Maoni ni mengi kwa mashabiki wake kufuatia kauli hiyo huku wengine wakidai alishaachika kitambo kwenye ndoa yake.

"Kuna muda natamani Ndoa... Ila nikikumbuka matukio hamu inaisha." Ameandika Irene na kuongeza, "Sema ndio hivyo hujui ulichopangiwa." - Ameandika @irenepaul001 Kufuatia kauli hiyo ya Irene Paul, huenda kwasasa ndoa yake haipo tena. Una lipi la kumshauri... 🤔

Fahamu, kitaaluma mwigizaji huyo mahiri ni mwanahabari na yupo kwenye tasnia ya filamu nchini kwa kipindi cha miaka 11 sasa. Pia ana brand yake inayojishughulisha na uuzaji wa bidhaa za nywele asilia na mwili inayoitwa "Naturali STAR".

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad