Issa Azam Chawa wa Diamond Platnumz Yupo Tayari Kumuacha Mke Wake Kwa Ajili ya Mondi

 Chawa Issa Azam amefunguka kwamba Yupo tayari kumuacha mke wake ateketee na Moto huku akimuokoa kwanza Diamond.


Ameeleza kwamba ikitokea kuna moto umewaka then Diamond pamoja na mke wake wanaungua yeye ataanza kumuokoa kwanza Diamond kisha atampeleka Hospital halafu ndio atarudi tena kumuokoa mke wake.



Amefunguka zaidi kwamba Wanawake hawawezi kukuheshimu kama huna hela, hivyo ni sawa kumuokoa Diamond, kwani anampa hela pamoja na Umaarufu ambao unasababisha aweze kuhudumia familia yake.


Issa amebainisha kwamba Diamond ni Rais wa Muziki hapa Tanzania hivyo atamlinda kwa nguvu na moyo wake wote, amesema ukitaka kumshambulia Diamond inabidi uanze na yeye kwanza.


Baada ya kauli hizi za Issa Azam, mjadala uliwekwa Twitter huku watu wengi wakimuona Issa kama mtu aliyerukwa na akili, kwamba inakuwaje aongee maneno ya kipuuzi kisa kulinda ukaribu wake na Mond.


Mbali na waliomponda pia kuna watu wameungana nae na wamesema ni sawa yeye kuongea hivyo maana Diamond anamsaada mkubwa kwake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad